Nuru FM

Viongozi wa Dini kuhimiza amani uchaguzi mkuu

14 October 2025, 10:02 am

Kiongozi wa Bakwata akizungumzia kuhusu umuhimu wa kuitunza amani. Picha na Ayoub Sanga

Wakati sahihi kwa viongozi wa dini kutoa ujumbe unaowaunganisha Watanzania, badala ya maneno yanayoweza kuchochea chuki au migawanyiko.

Na Ayoub Sanga

Waandishi wa habari na viongozi wa dini Mkoani Iringa wametakiwa kutumia nafasi zao kuhimiza amani na umoja wa kitaifa, hususan katika kipindi hiki kinachoelekea uchaguzi mkuu, ili kuepusha mifarakano na migawanyiko miongoni mwa Watanzania.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa mradi kutoka BAKWATA Makao Makuu, Bw. Omari Ibrahim katika warsha ya siku moja iliyoratibiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mjini Iringa kwa kushirikisha waandishi wa habari na viongozi wa dini kutoka madhehebu mbalimbali.

Sauti ya Omari Ibrahim

Kwa upande wake, Mchungaji Judith Sanga wa Kanisa la Glory to God Miracle Mission, ameipongeza BAKWATA kwa kuandaa semina hiyo na kusema kuwa amejifunza umuhimu wa kushirikiana kati ya viongozi wa dini na waandishi wa habari katika kueneza ujumbe wa amani na maadili kwa jamii.

Sauti ya Mchungaji

Naye mwandishi wa habari kutoka Matukio Daima, Francis Godwin, amesema semina hiyo imemkumbusha wajibu wa waandishi wa habari katika kutoa taarifa sahihi na zinazozingatia maslahi ya umma.

Sauti ya Mwanahabari

Semina hiyo imelenga kutoa elimu ya uraia kwa makundi hayo muhimu katika jamii ili kuongeza uelewa kuhusu wajibu wao katika kulinda amani, mshikamano wa kitaifa, na matumizi sahihi ya majukwaa ya mawasiliano katika kuelimisha umma.