Nuru FM
Nuru FM
24 September 2025, 9:49 am

“Vijana ndio hazina ya Leo hivyo wanapaswa kuchagua viongozi wanaowataka kwa maslahi Yao na Taifa” Alisema Mvamba
Na Hafidh Ally
Vijana Wilaya ya Iringa wameaswa kutokukubali kuathiriwa na taarifa za kupotosha zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwa lengo la kuwavunja moyo na kuwazuia kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni za uchaguzi katika Kata ya Lumuli, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Vijijini, Ndugu Arnold Mvamba, amesema baadhi ya watu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kusambaza taarifa zenye kuleta , taharuki , hofu na propaganda zinazolenga kuwakatisha tamaa wananchi hasa vijana, ili wasijitokeze kupiga kura ifikapo Oktoba 29, 2025.
Aidha amewataka kuchagua viongozi bora kwa kuwa kesho iliyobora inajengwa leo kwa kuchagua kiongozi mwenye kiu ya kuleta maendeleo.

Kwa upande wake Mgombea Udiwani wa CCM Kata ya Lumuli, Ndugu Abeid Kisinini amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kimeweza kuleta maendeleo hivyo ni wakati wa wananchi kuendelea kuwaamini kwani serikali imeboresha huduma za shule na Miundombinu ya Barabara.
Naye Mgombea wa Ubunge Jimbo La Kalenga Jackson Kiswaga amesema kuwa serikali imeendelea kufanya shughuli za kimaendeleo ikiwemo kusambaza umeme ambapo ni muda sasa wa wananchi kuwapa kura ya ndio katika uchaguzi mkuu ili wazidi kuwapatia maendeleo.