Nuru FM
Nuru FM
4 September 2025, 8:29 pm

Rushwa Imetajwa kuwa adui wa haki jambo linalopelekea Takukuru Iringa kutoa elimu.
Na Joyce Buganda
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Iringa imetoa elimu ya kujiepusha na Rushwa kwa wagombea wa Udiwani wa manispaa ya Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM wa kata zote 18 pamoja na viti maalumu.
Akizungunza wakati na wagombea hao katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Iringa Mjini zilizipo sabasaba, Mkuu wa Dawati la elimu kwa umma TAKUKURU Mkoa wa Iringa Bw. Ditram Mhoma amesema elimu hiyo ni endelevu na itatolewa kwa vyama vyote vya siasa katika kipindi hiki cha Kampeni kuelekea katika uchaguzi mkuu wa Oct 29 mwaka huu.
Kwa upande wao baadhi ya Wagombea wa Udiwani Kata za Manispaaa ya Iringa wamesema imekuwa kawaida kwa wananchi kudhani kuwa kumpigia kura mgombea ni lazima wapewee pesa jambo ambalo linachochea vitendo vya rushwa.
Ikumbukwe kuwa uchaguzi mkuu utafanyika tarehe 29 mwezi wa 10 mwaka 2025 huku wanachi wakihimizwa kuchagua viongozi watakaowafaa kuwaongoza kwa kipindi cha miaka 5.