Nuru FM
Nuru FM
18 August 2025, 10:51 am

Miradi ya maendeleo ikisimamiwa ipasavyo hadi kukamilika kwake itasaidia kukuza huduma bora za kijamii kwa wananchi.
Na Adelphina Kutika
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, amewataka Wakuu wa Taasisi ya TANROADS, TARURA, RUWASA na IRUWASA kuhakikisha wanasimamia ipasavyo miradi inayoendelea kutekelezwa mkoani hapa yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 617.
Akizungumza na wakuu wa taasisi hizo, kwenye kikao cha kutoa Taarifa ya ziara ya ukaguzi wa miradi aliyoifanya siku za hivi karibuni katika Halmashauri zote , Mhe. Kheri amesema kuwa fedha hizo zimetolewa na Serikali kwa lengo la kuboresha huduma za jamii, ikiwemo miradi ya barabara, maji na miundombinu mingine muhimu.

Aidha amesema kuwa katika mradi ya Maji kuna miradi 30 yenye thamani ya shilingi Bilion 70 katika mkoa mzima na RUWASA wanaendelea kusimamia kwa umakini ili iweze kuwanufaisha wananchi.
Mhe. Kheri amesisitiza utekelezaji wa miradi ufuate masharti ya mikataba ili kulinda maslahi ya wananchi na kuhakikisha huduma zinawafikia walengwa, pamoja na kuwataka viongozi wa mitaa na vijiji kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuitunza miundombinu iliyokamilika.
Hata hivyo Serikali ya mkoa itafanya ziara za mara kwa mara kuhakikisha fedha zinatumika ipasavyo na miradi inafikia malengo yake yaliyokusudiwa.