Nuru FM
Nuru FM
19 June 2025, 12:36 pm

Na Godfrey Mengele
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imetakiwa kufuatili kiasi cha shilingi Milion 212.4 kilichotolewa kwa ajili ya mkopo kwenye vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambapo fedha hizo hazirejeshwa.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la wilaya hiyo Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Peter Serukamba amesema kuwa taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali 2023/2024 inaonesha kuwa ni shilingi milion 1 kati ya fedha hizo ndio iliyorejeshwa.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Bi. Dorice Kalasa amemtaka Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Robert Masunya kuwachukulia hatua za kisheria watumishi waliosababisha hoja zenye viashiria vya ubadhirifu wa rushwa kwa mujibu wa ripoti kutoka Ofisi ya CAG.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Steven Mhapa amesema kuwa ili halmashauri hiyo ijiendeshe inatakiwa kukusanya mapato na kuyatumia ipasavyo hivyo uzembe wowote utakao jitokeza kwenye ukusanyaji wa mapato athari yake ni kuwa tegemezi.