Nuru FM
Nuru FM
8 June 2025, 5:35 pm

LATRA imesema kuwa Mchakato wa kupata leseni kwa madereva ni mwepesi hivyo wachangamkie fursa ya kupata leseni za usafirishaji.
Na Godfrey Mengele
Madereva pikipiki na bajaji Mkoa wa Iringa wametakiwa kukata leseni za usafirishaji kwa hiyari kabla ya hatua kuchukuliwa ili kuwasaidia pindi wapatapo matatizo katika utekelezaji wa majukumu yao.
Hayo yamezungumzwa na Joseph Umoti Afisa Mfawithi wa Latra Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri ardhini Mkoa wa Iringa na kubainisha kuwa leseni hizo zipo kwa mujibu wa sheria za usafirishaji za vyombo vya kukodi na umsaidia dereva pindi changamoto inapotokea ikiwamo kwa abiria.
Umoti amesema kuwa leseni ya pikipiki ya magurudumu mawili { bodaboda } Sh Elfu 17,000 kwa mwaka na leseni ya bajaji ni Sh Elfu 22,000 kwa mwakana kuwataka maafisa usafirisha kukata leseni kwa hiari kabla ya kuanza zoezi la kuwakamata wasiokata leseni.
Umoti amesema kuwa mamlaka imetanua wigo wa ukataji leseni ili kumsaidia mmiliki wa chombo kupata huduma kwa uharaka zaidi.
Tumezungumza na madereva wa Bajaji na pikipiki Manispaa ya Iringa na tumewauliza wanafahamu umuhimu wa kukata leseni ya usafirishaji maarufu kama stika ya Latra? Majibu yao yalikuwa hivi
Naye Mwenyekiti wa Bajaji wilaya ya Iringa UMABAI Bw. Melabu kihwele ametoa wito kwa madereva kukata leseni ya usafirishaji ili kuepuka faini.
MWISHO