Nuru FM
Nuru FM
14 April 2025, 11:14 am

Na Ayoub Sanga
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa Vijijini, Elia Juma Kidavile, ametoa wito kwa vijana wa wilaya hiyo kutotumika vibaya kwa maslahi binafsi ya wanasiasa na badala yake kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha uchaguzi mkuu ujao unafanyika kwa amani na utulivu.
Akizungumza na vijana wa kata ya Migoli, wilayani Iringa, wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji UVCCM, Kidavile alieleza umuhimu wa vijana kuwa chachu ya mabadiliko chanya na ulinzi wa amani, hasa katika kipindi nyeti cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025.

Aidha Kidavile amesema kuwa wanatamani kupata vijana wanaobeba ajenda za vijana ili kutatua changamoto zao katika jamii.
Naye Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa Vijijini, Omary Chulla, amesema kuwa vijana wanapaswa kuienzi tunu ya nchi ya amani kuelekea katika uchaguzi wa mwaka huu.
