

21 February 2025, 12:08 pm
Na Ayoub Sanga
Serikali kupitia wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA imetoa zaidi ya shilingi Millioni 271 kwaajili ya uboreshaji wa mradi wa maji wa Ruaha Mbuyuni wilayani Kilolo,mradi ambao unaenda kuondoa adha ya upatikanaji wa maji safi na salama.
Akizungumza wakati akishuhudia zoezi la utiaji saini, uboreshaji wa mradi wa maji wa Ruaha Mbuyuni Wilayani Kilolo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Serukamba ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha hizo zinazoenda kumaliza changamoto ya maji safi na salama huku akiwataka wakandarasi walio saini mkataba huo kufanya kazi kwa Haraka na kwa ubora ili kuwezesha Wananchi wa kijiji cha Ruaha Mbuyuni na Msosa kupata huduma ya maji safi na salama.
Mhe.Serukamba ameongeza kwa kuwasisitiza wakandarasi walio saini mkataba huo kufanya kazi kwa Haraka na kwa ubora ili kuwezesha Wananchi wa kijiji cha Ruaha Mbuyuni na Msosa kupata huduma ya maji safi na salama .
Aidha Mhe. Serukamba amewaagiza RUWASA na Tume ya Umwagiliaji Mkoa wa Iringa kuwasimamia ipasavyo wakandarasi wa miradi hiyo kwa kuhakikisha miradi inakamilika kwa Wakati.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Dkt. Ritta Kabati amesema kuwa serikali imekuwa na dhamira ya kumtua mwanamke ndoo Kichwani .
Kwa upande wao Wananchi wa Kijiji Cha Ruaha Mbuyuni wameishukuru Serikali Kwa kuwasadia kuboresha mradi huo wa Maji ambapo wamesema utakwenda kuwa Mkombozi kutokana na adha kubwa wanayoipitia kwasasa ya ukosefu wa maji safi na salama suala linapelekea kukwamisha shughuli zao za Kiuchumi.
Uboreshaji huo wa mradi wa maji wa Ruaha Mbuyuni utahudumia Vijiji Viwili vya Msosa na Ruaha Mbuyuni vyenye jumla ya watu wapatao 34,028.