DC Kheri: Serikali italinda uhuru wa kuabudu
14 November 2024, 9:22 am
Na Adelphina Kutika
Serikali mkoani Iringa imesema itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu pamoja na kutoa ushirikiano kwa dini zote.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kheri James katika mahafali ya kwanza ya kuwatunukia wahitimu 14 wa Stashahada, Shahada na Shahada ya Uzamili katika elimu ya theolojia kwenye chuo cha Corner Stone kilichopo Kata ya Gangilonga, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Kwa upande wa askofu Dkt Mpeli Mwaisumbe amewakumbusha wahitimu kuwa ni muhimu kufuata muongozo na sheria zilizowekwa na serikali ili kuepuka matatizo ya kisheria na kudumisha uhuru wa ibada.
Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Gwada ambaye yeye amewashauri wahitimu kutumia makanisa kama jukwaa la kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto, ambavyo vimekuwa changamoto kubwa katika Manispaa ya Iringa.
Nao baadhi ya wahitimu wa theolojia akiwemo lupyana samweli wameshauri serikali kufuatilia viongozi wa dini wanaotoa huduma pasipo kuwa na elimu.
Hata hivyo Ikumbukwe mahafali hiyo ni ya kwanza kwa chuo cha Corner Stone kinachoendelea kuiandika historia ya kuzalisha wasomi wa theolojia katika mkoa wa Iringa.
MWISHO