Serikali kuboresha miundombinu hifadhi ya taifa ya Ruaha
8 October 2024, 12:11 pm
Na Joyce Buganda
Serikali imapanga kuboresha miudombinu katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha Mkoani Iringa ili kuongeza idadi ya watalii kufika bila kero huku wawekezaji wakishauriwa kwenda kuwekeza hifadhini hapo.
Akizungumza katika kilele cha miaka 60 ya hifadhi ya taifa ya Ruaha Waziri wa Maliasili na utalii Balozi Pindi Chana ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu katika hifadhi za taifa ili kukuza utalii.
Peter Serukamba ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa amezipongeza sekta binafsi kwa kuwekeza katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo ina vivutio ambavyo havipatikani katika hifadhi nyingine.
Kwa upande wake muhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya ruaha Godwell Meingataki amesema historia imeandikwa kwani changamoto walizozipata wao wamezigeuza kuwa fursa ndo maana wanajivunia kufika miaka 60.
Hifadhi ya Kitaifa ya Ruaha inajulikana kwa idadi kubwa ya tembo (inakadiriwa kuwa zaidi ya 10,000) wanaokusanyika katika eneo moja kuliko eneo lingine lolote Afrika Mashariki na idadi nzuri ya wanyama walanyama.
MWISHO