Nuru FM

Viongozi wa dini wazuru hifadhi ya Taifa Ruaha

4 October 2024, 3:51 pm

Viongozi wa dini wakiwa na Mhifadhi wa hifadhi ya Ruaha. Picha na Adelphina Kutika

Na Adelphina Kutika

Viongozi wa dini kutoka Mkoa wa Iringa wamejizatiti kushirikiana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha katika kutoa elimu kuhusu uhifadhi wa vyanzo vya maji na ulinzi wa mazingira.

Haya yanajiri kufuatia  ziara ya viongozi October  3  2024 ndani ya hifadhi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuzaliwa  kwa hifadhi hiyo, ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini.

Wakati wa ziara, viongozi hao walishuhudia athari za shughuli za kibinadamu, uharibifu wa mazingira, na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha kupungua kwa kiwango cha maji kwenye Mto Ruaha Mkuu. 

Akizungumza Kwa niaba ya Shekh wa Mkoa wa Iringa Salum Mwahuta  alisisitiza umuhimu wa kulinda mto huo, ambao ni chanzo muhimu cha maji ndani ya hifadhi.

Sauti ya Sheikh

Kwa upande wake  Askofu Ezekiel Mwenda, Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa ya Kipentekosti Mkoa wa Iringa, alieleza wasiwasi wake kuhusu wananchi wanaoendeleza vitendo vya kupunguza maji katika vyanzo vya mto huo, hali inayochangia kukauka kwa mto katika msimu wa kiangazi.

Sauti ya Askofu

Afisa Mhifadhi Mkuu wa Ruaha, Rehema Kaitila, alieleza kuwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) tayari limeanza hatua za kukabiliana na tatizo la kukauka kwa Mto Ruaha. 

Sauti ya Mhifadhi

Nao baadhi ya waumini waliopata wa fursa kutembelea hifadhi hiyo  wamesisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kutunza rasilimali za maji na mazingira pamoja na kubadilishana mawazo juu ya umuhimu wa kutunza  Mto Ruaha na hifadhi hiyo unakuwa salama.

Sauti ya waumini

MWISHO