Nuru FM

Serukamba: Jitokezeni kujiandikisha daftari la wapiga kura

27 September 2024, 8:47 pm

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba akizungumza na wanahabari kuhusu uchaguzi wa serikali za Mitaa. Picha na Ayoub Sanga

Na Hafidh Ally

Wananchi mkoani Iringa wametakiwa kujitokeza kwa wingi  kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura  Kuelekea  uchanguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwezi November mwaka  huu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofsini kwake Mkuu wa Mkoa wa Iringa Peter Serukamba amesema kwa mujibu wa kanuni ya 9 GN. Na. 571 na kanuni ya. 8 GN Na.572  ya kanuni ya uchaguzi wa viongozi wa serikali Mitaa mwaka 2024.

Sauti ya RC

Amesema kuwa msimamizi wa uchaguzi amepewa mamlaka ya kutoa maelekezo  kuhusu uchaguzi ambayo yanatotewa siku 62 kabla ya siku ya uchaguzi.

Sauti ya RC

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Iringa Mjini, Kastori Msigala, amesema kuwa kwa mujibu wa kanuni wakazi wenye umri wa miaka 18 wanatakiwa kupiga kura na wale wanaotaka kugombea nafasi za kugombea wanatakiwa kuwa na umria kuanzia miaka 21.

Sauti ya Msimamizi

MWISHO