Wilaya ya Kilolo mguu sawa kwa uchaguzi serikali za mitaa
17 September 2024, 10:32 am
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unahusisha kuchagua viongozi kwenye nafasi za Mwenyekiti wa Kijiji, Mwenyekiti wa Kitongoji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Mchanganyiko) na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (Kundi la Wanawake).
Na Hafidh Ally
Kuelekea uchaguzi wa serikali za Mitaa hapa Nchini, Msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Hassan Juma Mnyikah ametangaza amri ya mgawanyo wa maeneo ya utawala katika Wilaya hiyo.
Mnyikah amesema wilaya ya kilolo ina mamlaka ya mji mdogo ambayo ni ilula,kata 24,vijiji 94 na vitongoji 484 na ndiyo maeneo yatakayo Shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa wakiwemo wenyeviti wa vijiji , vitongoji na wajumbe wa serikali za vijiji wasio zidi 25 kwa kila kijiji.
Aidha amewataka viongozi wa Wilaya ya Kilolo kushirikiana katika kuwahamasisha wananchi wao kujiandikisha ili waweze kupiga kura.
Katika hatua nyingine Hassan ameishukuru serikali kwa kufanya maandalizi makubwa yatakayosaidia wananchi kuwachagua viongozi wanaowataka na watakaowaletea maendeleo.
Uchaguzi wa serikali za Mitaa unaenda kufanyika Nov 27 2024 ambapo Kauli mbiu inasema serikali za mitaa, sauti ya wananchi , jitokeze kushiriki uchaguzi.
MWISHO