Nuru FM

Manispaa ya Iringa kuhuisha usajili wa bajaji

5 June 2024, 11:33 am

Baadhi ya Madereva wa bajaji Manispaa ya iringa. Picha na Azory Orema

Hatua ya Serikali ya kuweka mfumo mpya wa usajili wa namba za pikipiki na bajaji inalenga kuweka mfumo na utaratibu mzuri wa uratibu wa vyombo hivyo vya usafiri kwa lengo la kuhakikisha usafiri huo unakuwa salama, ikiwa ni pamoja na kupunguza uhalifu na ajali za barabarani.

Na Azory Orema

Baadhi ya madereva bajaji Manispaa ya iringa wameonesha kupokea maagizo yaliyotolewa na Halmashauri ya Manispaa juu ya kuhuisha usajili wa bajiji zao.

Wakizungumza na nuru fm madereva hao wamesema kuwa zoezi hilo la kuhuisha usajili wa bajiji hizo utasaidia watu kutokufuata sheria na kuepusha vitendo vya uhalifu ndani ya manispaa na mkoa kwa ujuimla.

Sauti ya Madereva

Kwa upande wake Mwenyekiti wa madereva bajaji Wilaya ya Iringa melabu kiwele amesema kauli iliyotolewa na Halmashauri inalenga kuhuisha usajili wa bajiji na sio kusajili upya bajaji hizo.

Sauti ya Mwenyekiti Bajaji

Sanjari na hayo Melabu amesema zoezi hilo litasaidia kuwatambua madereva bajaji na vyombo vyao ili kuepuisha sintofahamu yeyote inayoweza kujitokeza.

Itakumbukwa tarehe 23/5/2024 halmashauri ya Manispaa ya Iringa chini ya Mstahiki Meya Ibrahimu Ngwada aliagiza kuaza upya zoezi la kusajili bajaji zote zinazofanya kaz ya usafirishaji ndani ya manispaa.