Polisi Iringa watoa tamko wizi wa mifugo
17 May 2024, 8:54 am
Wizi wa mifugo umekuwa desturi iliyoenea na wakati mwingine inayosababisha wafugaji kuwa maskini jambo lililopelekea jamii hiyo kuazimia namna ya kukabiliana na changamoto.
Na Joyce Buganda
Wizi wa mifugo watajwa kuwa kikwazo kikubwa kwa wadau wa ufugaji mkoani iringa huku wafugaji wakitakiwa kuwa na ushirikiano na jeshi la polisi ili kukomesha yabia hiyo.
Akizungumza kwenye kikao cha wafugaji na jeshi la polisi kamishna msaidizi, mwandamizi wa jeshi la polisi na Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi amesema ili kukomesha tabia hiyo inatakiwa kila mfugaji afanye utafiti wa mifugo.
Naye Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa iringa Riziki Makwaya amesema kwa kipindi cha Januari mpaka Aprili kwa mwaka huu ni matukio 14 ya uhalifu yameripotiwa hivyo matukio yamepungua kwa kiasi kikubwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Wilaya ya Iringa Emanuel Sairuti amesema wataendelea kutoa ushirikiano na jeshi la polisi ili kutokomeza na kumaliza kabisa.
MWISHO