Nuru FM

Afande Mwaipopo: Wekeni viakisi mwanga kupunguza ajali

16 May 2024, 11:30 am

Maafisa wa usalama barabarani Mkoani Iringa wakizungumzia kuhusu Viakisi mwanga Nuru fm. Picha na Hafidh Ally

Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoa wa Iringa kimeanza kutoa elimu ya umuhimu wa kuweka viakisi mwanga kwenye magari ili kupunguza ajali za barabarani hasa kwenye maeneo hatarishi nyakati za usiku.

Na Hafidh Ally

Madereva wa vyombo vya moto wameshauriwa kuweka viakisi mwanga katika magari yao kwa mujibu wa sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali.

Hayo yamezungumzwa na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi  Yasinta Mwaipopo alipokuwa akizungumza na Nuru fm kuhusu kanuni na taratibu za viakisi mwanga vyenye lengo la kusaidia madereva kuchukua tahadhari hasa nyakati za usiku.

Sauti ya Afande Mwaipopo

Kwa upande wake Meja Magreth amesema kuwa viakisi mwanga vinatakiwa kuwekwa katika magari kutokana na utaratibu ambao wamewaelekeza madereva.

Sauti ya Meja Magreth

Naye Balozi wa usalama barabarani Mkoani Iringa iringa Emanuel Fungo amewasihi madereva wa vyombo vya moto kutowasha taa full wakati wa usiku ili kuwalinda watumiaji wengine wa barabara na ajali.

Sauti ya Fungo

MWISHO