Zao la chai lapanda thamani Iringa
10 May 2024, 12:24 pm
Zao la chai limeandaliwa mikakati ili kuwanufaisha wakulima na wadau wa zao hilo Mkoani Iringa.
Na Joyce Buganda
Wadau wa chai nchini wametakiwa kutoyatelekeza mashamba yao ya chai kwani kwa sasa zao hilo limeonekana kufumuka upya kwa uthamani pamoja na bei nzuri.
Akizungumza katika kikao cha viongozi wa vyama vya ushirika vya wakulima wadogo wadogo kilichofanyika katika chuo kikuu huria mkoani Iringa Mkurugenzi Mkuu, wakala, Maendeleo ya wakulima wadogo wa chai Ɓw. Theophord Ndunguru amesema wakulima wengi wa chai wamekuwa wakiyatekeleza mashamba yao bila kuyahudumia pamoja na kuyabadilishia matumizi kwa kuamini zao hilo limeshuka thamani.
Muwakilishi kutoka Tanzania Fertilizer Company kampuni ya mbolea Tanzania ( TFC) Bw. Daud Siarra amesema hii ni taasisi ya ya kiserikali inafanya kazi na vyama vya ushirika vyote nchini hivyo wanahitaji kujua mbolea gani imahitajika kwenye zao la chai.
Kwa upande wake Joshua Ngo’ndya Meneja wa mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) nyanda za juu kusini wao wao ndio wanaothibiti ubora wa mbolea ili wakulima wapate mbolea bora kuanzia inapotengenezwa mpaka inapotumika kwa wakulima, huku akisema vita ya urusi ukraine viliathiri sana upatikanaji wa mbolea jambo ambalo lilifanya viwanda vingi kusua sua kufanya kazi.
Akiongea kwa niaba ya wajumbe waliohudhulia kikao hicho mmoja wa wajumbe hao wameiomba serikali kutoa bei elekezi kwa wakulima lakini wanaomba mbolea ipatikane kwa wakati.
MWISHO