Nuru FM

Serikali kuboresha miundombinu ya elimu Iringa

2 May 2024, 9:46 am

Serikali inatambua haki ya kila mtu kupata elimu na hivyo inawekeza katika kuweka mifumo na miundombinu stahiki ya kielimu Kwa ajili ya wanafunzi nchini.

Na Joyce Buganda

Serikali imedhamiria kuendelea kuimarisha sekta ya elimu Kwa kuimarisha miundombinu na kuboresha stahiki za walimu kwa kuongeza vitendea kazi na nyenzo nyingine. 

Hayo yamezungumza na Mkuu wa wilaya ya Iringa Komred Kheri James wakati wa alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua ujenzi na mwenendo wa masomo katika shule ya Sekondari shabaha ambapo ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya sita itaendelea kuongeza vitendea kazi na kusimamia ushiriki wa wazazi katika mageuzi na ustawi wa sekta ya elimu wilayani Iringa.                 

Sauti ya DC Heri

Aidha Kheri James amewaasa wanafunzi kusoma kwa bidii pindi wawapo shuleni kujenga kizazi chenye maadili na misingi bora na kujitegemea.

Sauti ya DC Heri

Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi shuleni hapo wameishukuru serikali kwa maboresha ya shule yanayofanywa hivyo sasa tofauti na awali.

Sauti ya Wanafunzi

MWISHO