Zaidi ya miche 2,000 yapandwa kijiji cha Ulole
3 April 2024, 9:57 am
Licha ya serikali kuwa na utaratibu wa kupanda miti mara kwa mara bado kumekuwa na tabia ya wananchi kuharibu huku serikali ikapanga kuwachukulia hatua wanaokata miti ovyo.
Na Adelphina Kutika
Zaidi ya miche 2,000 ya miti rafiki na maji imepandwa katika vyanzo vya maji kwenye vijiji vinne vinavyozunguka shamba la miti Saohill wilayani mufindi Mkoani Iringa ili kurejesha uoto wa asili na kuhuisha mtiririko wa maji.
Wakizungumza katika zoezi la upandaji wa miti katika chanzo cha maji Nyamangile kilichopo kijiji cha Ulole ambacho kinahudumia wananchi zaidi ya elfu moja baadhi ya wananchi wanasema uhifadhi wa vyanzo vya maji umeanza kuonesha dalili njema.
Kwa upande wake Mhifadhi mkuu shamba la miti SAOHILL PCO TEBBY YORAMU amesema lengo lakutoa miche hiyo nikusaidia wananchi kuendelea kuhifadhi vyanzo vya maji.
Awali akizungumza na wananchi wa kijiji cha ulole mkuu wa wilaya ya mufindi Dr. Linda Salekwa amesema serikali inaendelea kuwachukulia hatua wale wote watakaobanika kuharibu vyanzo hivyo ikiwemo kufanya shughuli za kibinaadamu ikiwemo kilimo.
Shamba la miti SAOHILL ni miongoni mwa mashamba ishirini na nne ya serikali ,likiwa ndio shamba kubwa likijumuisha hekta elfu arobaini na nane na mia mbili ni misitu ya asili na hekta elfu themanini na sita ni za miti ya kupandwa.