Madereva daladala Iringa wagoma tena
13 March 2024, 9:32 pm
Serikali inatakiwa kufanyia kazi malalamiko ya muda mrefu ya Madereva wa Daladala ambayo yamekuwa kero kwa watumiaji.
Na Azory Orema
Wananchi wanaotumia usafiri wa daladala Manispaa ya Iringa wamelalamikia ugumu wa usafiri wao baada ya daladala zinazopakia abiria kugoma kufanya kazi.
Wananchi hao wamesema hali ya biashara sio nzuri huku wakiomba serikali kufanyia kazi malalamiko ya muda mrefu ya Madereva wa Daladala ambayo yamekuwa kero kwa watumiaji.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa madereva Daladala Manispaa ya Iringa Ndugu Rashid Ayubu amesema mgomo wa daladala unatokana na Bajaji na Viongozi wa Serikali kushindwa kusimamia makubaliano.
Rashid amesema licha ya daladala kutii sheria na makubaliano lakini bado hakuna usawa baina vyombo vyao na bajaji.
Mwaka Jana Madereva hao waliwahi kugoma wakishinikiza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuwazuia Madereva bajaji kupita katika njia ambazo wao wanazitumia jambo ambalo Bado limeshindwa kitafutiwa ufumbuzi.
MWISHO