Nuru FM

Wilaya ya Iringa kuongeza Bajeti ya Majosho ya Mifugo.

30 January 2024, 7:48 pm

Halmashauri ya wilaya ya Iringa imejipanga kuhakikisha inajenga majosho katika maeneo mbalimbali ili kuwarahishishia wafugaji kutotembea umbali mrefu kwa ajili ya kuipeleka mifugo maeneo ya majosho yalipo.

Hayo yamezungumzwa katika Baraza la Madiwani la Madiwani la Halmashauri hiyo lilipoketi kwa ajili ya kupitisha bajeti ya mwaka 2024/2025 ambapo miongoni mwa hoja zilizojadiliwa ni pamoja na changamoto ya uhaba wa majosho kuwa machache kulinganisha na wingi wa mifugo iliyopo.

Akitoa hoja hiyo wakati wa kujadili idara ya kilimo, Mifugo na uvivu, Diwani wa Kata ya kihanga Ndg Hamis Nziku amesema kuwa ndani ya kata yake kuna takribani wafugaji 25 lakini wanategemea Josho moja hivyo kuiomba halmashauri hiyo katika utekelezaji wa bajeti ya 2024/2025 ni vyema kujenga josho ndani ya kata yake ili kuwasaidia wafugaji hao.

Akijibu hoja hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa amesema kuwa ndani ya Halmashauri hiyo ipo changamoto ya Majosho hivyo katika bajeti hii kuna umuhimu wa kuongeza idadi ya majosho kwa ajili ya Mifugo.

“…Si kata yako tu ya kihanga Mheshimiwa diwani suala ya majosho ni halmashauri nzima kuna changamoto kwa sasa lazima tukubali tuna wajibu wa kukabiliana na hili tujenge majosho katika maeneo mbalimbali kwani Wafugaji kwenye halmashauri hii ni wengi lakini idadi ya majosho ni ndogo katika bajeti hii tutajitahidi kujenga….”