Nuru FM

Wanafunzi 11, mwalimu wapigwa na radi Iringa

15 January 2024, 3:23 pm

Mkuu wa Mkamoa wa Iringa Halima Dendego akizungumza na wahanga wa tukio la kupigwa na Radi. Picha na Godfrey Mengele.

Na Godfrey Mengele

Jumla ya wanafunzi 11 na mwalimu mmoja wa shule ya Msingi Uyole iliyopo Halmashauri ya manispaa ya iringa wamepigwa na radi asubuh ya leo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Halima Dendego alipofika katika hospitali ya Rufaa Mkoa wa Iringa kuwajulia hali waathirika hao amesema mara baada ya kutokea kwa tukio hilo zilifanyika jitihada mbalimbali kuwahudumia wahanga hao.

Kwa upande wake Dr Huruma Mwasipu Mkuu wa Idara ya magonjwa ya dharula Hospitali ya rufaa Mkoa wa Iringa amesema kuwa wahanga hao wa kupigwa na radi walifikishwa wakiwa na majeraha madogo madogo wamepatiwa matibabu huku wengine wakitajia kuruhusiwa.

Dr Hamza Mwamuhehe ni Diwani wa Kata ya kitwiru anasemea majira ya asubuh hali ya hewa ilibadilika ghafla ndipo mvua ilipoanza kunyesha ikiambatana na radi zilizopigwa na kuwakuta wanafunzi na mwalimu wao wakiwa darasani na kusababisha madhara hayo.

Mshahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ngwada kufuatia tukio hilo ametoa rai kwa wazazi na wananchi wa maeneo ya kitwiru kutolihusisha na imani za kishirikina kwani jambo hilo ni kawaida kutokea ila tahadhari zaidi zinapaswa kuchukuliwa.

Madhira hayo wamewakuta wanafunzi wa Shule ya msingi uyole ikiwa ni shule mpya huku lengo la kujengwa na shule hiyo ikiwa ni kupunguza ajali walizokuwa wanapata wanafunzi kwa kuvuka barabara kwenda upande wa pili inayopatika shule nyingine.

MWISHO