Mradi wa USAIDS Kizazi Hodari wawafikia watoto 9000 Iringa na Njombe.
14 November 2023, 4:12 pm
Na Denis Nyali
Jumla Ya Watoto 9000 Walioambukizwa Virusi Vya Ukimwi Wamefikiwa Na Mradi Wa USAIDS Kizazi Hodari Unaotelelezwa Kwa Mkoa Wa Iringa Na Njombe Na Kuwaunganisha Na Vikundi Mbalimbali Katika Kuwawezesha Kupata Kiuchumi.
Akizungumza Na Nuru Fm Mkurugenzi Wa Mradi Huo Doroth Matoyo Amesema Mradi Huo Unaofanya Kazi Ya Kuwasaidia Watoto Walioambukizwa Virusi Vya Ukimwi Na Kuwaunganisha Watoto Kwa Taassisi Za Dini Pamoja Na Vituo Vya Lishe Ili Kuwawezesha Kutimiza Ndoto Zao Na Kuongeza Kuwa Jumla Ya Watoto 9000 Wamefikiwa Na Mradi Huo.
Bi Matoyo Ameongeza Kuwa Kumekuwa Na Chanagamoto Ya Baadhi Ya Watoto Kutoikubali Hali Ambapo Wao Kama Mradi Wamekuwa Na Utaratibu Wa Kuwaunganisha Na Wafanyakazi Wa Ngazi Ya Jamii Pamoja Na Wataalamu Wa Afya Pamoja Na Wanasaikolojia.
Katika Kukabiliana Na Changomoto Za Kiuchumi Na Kuwawezesha Kujitegemea Mradi Umewaunganisha Wazazi Na Walezi Katika Vikundi Vya Kukopa Vya Halamashauri Kupata Mikopo Ya Wanawake Kupitia Vikundi Mbalimbali Ili Kuwawezesha Kiuchumi.