Wanafunzi 300 wanufaika na program ya kilimo-viwanda scholarship
20 October 2023, 10:08 pm
Na Adelphina Kutika
Zaidi ya Wanafunzi 300 wanaosomea kilimo katika vyuo Vinne vilivyo Chini ya programu inayojulikana kama Kilimo-Viwanda scholarship, wamenufaika na ufadhili wa masomo unaotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) nchini Tanzania.
Akiongea 19 Oktoba, 2023 wakati wa zoezi la ugawaji Vyeti Kwa wafadhiliwa wa Program hiyo iliyofanyika katika chuo cha Kilimo cha Mt. Maria goreth kilichopo kata ya Ilula halmashauri ya wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa , Mkurugenzi wa SBL Obinna Anyalebechi amesema ,programu hiyo inawalenga wanafunzi wanaotoka katika familia duni ambazo hazina uwezo wa kuwalipia ada watoto wao na kuongeza kuwa itasaidia kuongeza wataalamu wa kilimo.
Kwa mujibu wa Meneja Mahusiano na Mratibu wa Programu ya Kilimo-Viwanda scholarship kutoka kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Neema Temba Amesema,ni sehemu ya mkakati wa SBL wa kuongeza kiasi cha nafaka ambacho kampuni hiyo inanunua kwa ajili ya uzalishaji wa bia ambazo ni pamoja na mahindi, shayiri na mtama.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Kilimo Cha Mt. Mariagoreth Isaya Kigava, amewashukuru SBL kwa ufadhili wanaotoa na kuzitaka taasisi binafsi kuweza kujitokea na kusaidia sekta ya kilimo ambayo ni sekta mama nchini Tanzania.
Aidha baadhi ya wanafunzi wanaofadhiliwa na kampuni ya SBL Kupitia Program ya Kilimo –Viwanda Scholarship wameeleza namna wanavyonufaika na ufadhili huo kwani inawapa fursa ya kuwa maafisa ugani katika taasisi binafsi na serikali.