Wananchi Boma la ng’ombe wafurahia miundombinu ya barabara, zahanati
20 July 2023, 11:49 am
Na Hafidh Ally
Wananchi wa kata ya Bomalang’ombe wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wameishukuru serikali kwa kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo barabara, zahanati na shule.
Wakizungumza na Nuru FM baadhi ya wananchi wa kata hiyo wamesema kuwa kwa sasa miundombinu ya barabara imekuwa mizuri kwa kiwango cha lami huku wakishukuru pia kupata huduma bora za afya.
Kwa upande wake Diwani wa Viti Maalum tarafa ya Kilolo Mh. Regina Mleva amesema kuwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika eneo lao ni ushirikiano uliopo kati ya viongozi na wananchi.
Akizungumzia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata ya Bomalang’ombe diwani wa kata hiyo Mh. Odino Mwamgumba amebainisha kuwa miundombinu ya barabara na huduma za afya zinatolewa kwa wananchi.