Nuru FM
Mwili wa Kichanga waokotwa katika dampo la taka Iringa
17 May 2023, 3:37 pm
Na Ansgary Kimendo
Mwili wa mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na miezi tisa umekutwa ndani ya mfuko katika dampo lililopo eneo la kihesa sokoni kata ya Kihesa manispaa ya Iringa asubuhi ya leo.
Wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema, mwili huo umegunduliwa na kijana ambaye hujitafutia riziki kwenye majalala ambapo alikuta mfuko umefungwa na alipojaribu kufungua ndipo alipoona mwili huo.
AGUSTINO KIMILIKE ni mwenyekiti wa mtaa wa Sokoni amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa hilo si tukio la kwanza kutokea na wanaofanya si wakazi wa eneo hilo.
Aidha amesema kuwa wanawake wamekuwa wakitekeleza matukio hayo licha ya elimu kutolewa kwa wingi.
MWISHO.