Kihenzile Akabidhi Ng’ombe wenye thamani ya Million 51 Nyololo na Maduma.
23 April 2023, 3:47 pm
Dhumuni la ugawaji wa Ng’ombe hao ni kuhamasisha mnyororo wa maendeleo kwa wananchi wa Jimbo la Mufindi kusini na kutekeleza ahadi alizowaahidi wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Na Mwandishi wetu
Mbunge wa Mufindi kusini Mh. David kihenzile amekabidhi mradi wa ng’ombe wenye thamani ya Shillingi Million 51 unaotekelezwa na Shirika la World Vision kwa vikundi vya wafugaji vilivyopo kata ya Nyololo na Maduma.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Ng’ombe hao, Kihenzile amesema kuwa World Vision ambao mradi wanatekeleza Mradi huo wametoa ng’ombe kumi na tisa (19) ambapo madume kwa ajili ya mbegu kumi na tano (15) na pia amekabidhi mitamba wa nne (4) waliopandishwa na mbegu bora.
Hata hivyo Mh. Kihenzile amekabidhi pesa taslismu kiasi cha laki tano kwa vikundi hivyo ili ziwasaidie kusafirisha mifugo hiyo.
Zoezi hili liliongonzwa na Mbunge kihenzile sambamba na timu ya wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi iliyokuwa na Afisa wa Mifugo wa Halmashauri pamoja na Daktari wa mifugo wa halmashauri na muwakilishi kutoka kwenye shirika la World Vision lililopo Nyololo.
“Mmepata nafasi ya bahati ambayo ambayo viongozi wengi walitamani kupitiwa na mradi huu lakini umekuja kwentu Mufindi kusini hivyo inatakiwa tuutunze na kuuthamini mradi hii pia tuweze kuonyesha juhudi katika kuongeza bidii ya utendaji wa kazi ili tuweze kupata Zaidi miradi ya kimaendeleo katika kata zetu” alisema Mbunge wa jimbo la Mufindi kusini David kihenzile
Katika hatua Nyingine Mbunge kihenzile amewataka wanufaika wa mradi huo Pamoja na wafugaji wa kawaida kuwa na mazoea ya Kuzingatia Lishe Bora kwani Iringa imekuwa ni miongini mwa mikoa yenye Vyakula na Mifugo mingi ila inakabiliwa na tatizo na Utapiamlo na udumavu.
Naye Daktari wa Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Innocent Ng’oma amebainisha kuwa Ng’ombe waliotolewa wamefanyiwa vipimo maabala na kupewa chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa kuharibika kwa mimba.