Viongozi wa Dini na Serikali waungana Kupinga ulawiti na Ushoga Iringa
20 April 2023, 2:50 pm
Matukio ya ulawiti na Ushoga yamezidi kukithiri katika Jamii jambo lililopelekea Viongozi wa Dini na Serikali kukemea vikali.
Na Hafidh Ally
Viongozi wa Dini na serikali Mkoani Iringa wameungana kupinga vita vitendo vya ulawiti na ushoga ambavyo ni kinyume na maadili ya Kitanzania.
Akizungumza mara baada ya Kumalizika kwa mashindano ya Tisa ya Quran nyanda za juu kusini yaliyofanyika ukumbi wa Masiti Grand Hall Manispaa ya Iringa Kadhi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Sheikh Aboubakar chalamila amesema kuwa ni bora tukapinga vitendo vya ushoga na ikiwezekana kukataa misaada wanayoitoa kwa kigezo cha kusambaza utamatuni ambao haukubaliki hapa nchini.
Kwa upande wake Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa Ibrahim Ally Ngwada amesema kuwa ni vyema wazazi wakasimamia malezi bora kwa watoto ili kuwaepusha na vitendo vya ulawiti na ushoga.
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni amesema kuwa ni vyema wazazi wakawalea watoto katika mazingira bora ikiwemo wazazi wenyewe kuwa na maadili mema.
MWISHO