Waziri Masauni awataka Wazazi kusimamia maadili kwa watoto
17 April 2023, 12:08 pm
Maadili yameshuka kwa Kasi hivyo ni jukumu la wazazi na walezi kuwalea watoto kwa kufuata misingi ya Dini.
Na Hafidh Ally
Wazazi wametakiwa kuwale watoto katika Maadili Mema ili kuwaepusha watoto na matukio ya ukatili dhidi ya watoto yanayosababishwa na Mmomonyoko wa maadili.
Hayo yamezungumzwa na Naibu waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mh. Hamad Masauni alipokuwa mgeni Rasmi katika mashindano ya kuhifadhi Quran Nyanda za Juu kusini yaliyofanyika Ukumbi wa Masiti Grand Hall Manispaa ya Iringa na kuongeza kuwa wazazi na walezi wanajukumu la kuwalea watoto katika misingi ya Dini.
“Ni vyema wazazi Mlioko humu ndani mkahakikisha mnawalea watoto katika maadili mema na kufuata misingi ya Quran ili watoto wawe salama kwa sababu ya kuwa kizazi bora cha baadaye” alisema Wazir Masauni.
SAUTI 1 MASAUNI
Kwa upande wake Kadhi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Shekh Aboubakar Chalamilla amesema kuwa ni vyema wazazi wakahakikisha wanalea vijana kwa kuhakikisha wanahifadhi Quran ili iwasaidie katika kuwaongoza kimaadili.
Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Quran shekh Mudathir Issa Yoyota amebainisha kuwa kamati hiyo imefanikiwa kuimarisha uhusiano na Taasisi mbalimbali za kidini na kuongeza kiwango cha kuhifadhi Quraan kwa watoto.
Naye Shamsi Elmi Katibu wa Taasisi ya Dhi Nureyn Islamic Foundation Mkoani Iringa ambayo imekuwa wadhamini wa mashindano ya Quran Nyanda za Juu kusini amesema kuwa Taasisi yao imekuwa bega kwa bega kuhakikisha wanashirikiana na serikali kutekeleza shughuli za kijamii ikiwemo kujenga misikiti, shule, zahanati na kuchimba visima vya maji.
MWISHO