CCM Iringa Yatekeleza miradi ya afya na kilimo
22 March 2023, 9:22 am
Miradi inayotekelezwa Mkoani Iringa na serikali ni pamoja na miradi ya afya na Kilimo.
Na Adelphina Kutika
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Iringa kimeendelea kutekeleza miradi ya maendeleo nchini ikiwemo sekta ya afya na kilimo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Daudi Yasini, serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kuboresha Ujenzi wa vituo vya afya, hospital za wilaya, na za Rufaa
“Mbali na sekta ya afya serikali Sserikali imeongeza upatikanaji wa pembejeo za kilimo” alisema Yassin.
Baadhi ya viongozi wa serikali na taasisi binafsi wameeleza hisia zao juu ya uongozi huo mahiri wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha miaka miwili.
Wakizungumzia kupungua kwa gharama za pembejeo za kilimo baadhi ya wananchi katika manispaa ya Iringa wameeleza namna ilivyowapunguzia makali ya maisha .
Hayo yanajiri wakati Tanzania ikiadhimisha miaka miwili ya rais samia suluhu madarakani baada ya mtangulizi wake Hayati Dr John Pombe Magufuli.
MWISHO.