Usiri ndani ya familia chanzo cha ukatili Iringa
22 March 2023, 9:09 am
Katika kukabiliana na matukio ya ukatili katika jamii, usiri umetajwa kusababisha matukio hayo kukithiri.
Na fabiola Bosco
Usiri ndani ya familia umetajwa kuwa sababu ya ongezeko la vitendo vya ukatili wa kingono na vipigo kwa watoto mkoani Iringa licha ya elimu kutolewa katika jamii.
Kwa mujibu wa afisa maendeleo ya jamii manispaa ya Iringa Bi Suzan Nyagawa watoto wamekuwa wakifanyiwa ukatili ndani ya familia huku wazazi na watu wanaowazunguka wakishindwa kutoa taarifa za matukio hayo .
CUE 001 SUZAN NYAGAWA
Ameongeza kuwa ni vyema watoto wakatoa taarifa kwa viongozi wa serikali za mitaa na watu wa malezi ili kudhibiti vitendo hivyo .
“kwa kweli ni vyema wananachi wakawa wazalendo katika kutoa taarifa za ukatili zinapotokea katika maeneo yao” alisema Nyagawa
“kwa kweli ni vyema wananachi wakawa wazalendo katika kutoa taarifa za ukatili zinapotokea katika maeneo yao” alisema Nyagawa
Mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake wa kike alifanyiwa ukatili wa kingono anasema aliamua kutoa taarifa kituo cha polisi ili kudhibiti vitendo hivyo .
Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa Dkt. Arfred Mwakalebela kati ya watoto wawili hadi watatu wanaofikishwa hospitalini hapo kwa wiki wanakuwa wamefanyiwa ukatili wa kingono.
MWISHO