Elimu Matumizi Mitandao kwa Watoto
13 March 2023, 12:57 pm
Kutokana na kukua kwa teknolojia wazazi wametakiwa kuwafundisha watoto wao matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.
Na Joyce Buganda.
Mtaalamu wa masuala ya teknolojia na Tehama wilayani Mufindi Bw. Hasan Chunya amesema juu ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwa watoto kuwa yanaathiri ukuaji wao.
Bw. Hassan Chunya amesema elimu ya udhibiti wa matumizi ya mitandao kwa watoto ni lazima itolewe kwa wazazi na walezi ili iwaongozee vyema pindi wanapohitaji kuitumia.
Kwa upande wake Evance Msosi ambae ni mzazi wa kiume amesema kukua kwa teknolojia kunasabibisha wazazi kuwa nyuma kwenye ulimwengu wa kidigitali hali ambayo imepelkea watoto kuwa walimu kwa wazi wao.
Nao baadhi ya vijana wamesma kwa kadri wanavozidi kutumia mitandao ya kijamii wanaona inawza kuwaletea matokea chanya hivyokinachohitajika ni udhibithi wa matumizi yasio sahihi.