Wasanii Wakemea Ukatili Iringa
13 March 2023, 12:21 pm
Kufuatia matukio ya kikatili yanayoendelea kushamiri katika mkoa wa Iringa wasanii wenye asili ya Iringa wameamua kuungana kutengeneza filamu yenye maudhui ya kupinga ukatili.
Na Adelphina Kutika.
Wasanii maarufu wa filamu nchini ambao asili yao kutoka mkoa wa Iringa wamesema wapo katika hatua za mwisho za kuandaa filamu ambayo maudhui yake yatakuwa kupinga ukatili wa kijinsia uliokithiri mkoani hapa.
Akizungumza na kituo hiki Mwenyekiti wa taasisi ya shada organization inayojishughulisha na masuala ya kupinga ukatili wa kijijnsia nchini Halima Yahya Mpinge maarufu kama (DAVINA) amesema kuwa wamekwisha kuanza maandalizi ya awali ya kuandaa filamu hiyo ili kutoa elimu kwa umma kama sehemu ya kuunga mkoani juhudi za serikali awamu ya sita kwenye mapambano dhidi ukatili wa kijinsia .
“watoto wanaangamia sasa hivi,watoto wadogo wanafanyiwa vitendo vya kikatili,watoto wakiume wanaharibiwa wakiwa wadogo ,kwahiyo wazazi tuungane kukemea haya matendo taifa linaangamia”alisema
Shamsa Ford ni Mwenyekiti Mweza wa Tasisi ya Shada Organization amesema kuwa kutokana na tatizo la ubakaji na Ulawiti kuwa kubwa wameamua kushirikiana na wasanii wa mkoa wa Iringa kuhakikisha wanaanda filamu itakayotoaelimu ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Filamu mkoa wa Iringa Hamis Nurdin amesema kuwa lengo la kutengeneza filamu hiyo ni kwajili ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia na ulawiti.
wazazi tuungane kukemea haya matendo taifa linaangamia.