Uvutaji Sigara Sababu Mdomo Sungura
21 February 2023, 12:53 pm
Madaktari Bigwa kutoka mkoani Arusha wakishirikiana na shirika la THE SAME QUALITY FOUNDATION kutembelea mikoa mbalimbali kutibu.
Na Joyce Buganda.
Wajawazito na wazazi wenye watoto waliozaliwa na mdomo wazi wameshauriwa kutembelea vituo vya afya ili kujua maendeleo ya afya zao.
Akizungumza na kituo hiki Daktari Bingwa wa Upasuaji James Mbele amesema kuwepo kwa viini tete kwenye familia ni mojawapo ya sababu ya kuzaliwa mtoto mwenye mdomo wazi (mdomo sungura)
Daktari Bingwa wa Upasuaji Atanas Masele amesema wanafanya kazi kwa kushirikiana na shirika la THE SAME QUALITY FOUNDATION na wanafanya kazi pia mikoa yote Tanzania.
Nao baadhi ya wazazi ambao watoto wao wamepata huduma ya upasuaji wa mdomo wazi wamesema matibabu hayo yanawasaidia watoto wao kuchangamana na watoto wenzao na kuwaepusha na athari zinazotokana na unyanyapaa.