Wizara ya Maji Yaikumbuka Ilalasimba
17 February 2023, 4:19 pm
Ujenzi wa mradi huo wa bwawa la Ilalasimba katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa uliofanyiwa upembuzi yakinifu tangu mwaka 2018 sasa watarajiwa kujengwa.
Na Hawa Mohammed.
Zaidi ya shilingi bilioni mbili (2) zimetengwa na Wizara ya maji kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa maalum kwa shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo cha umwagiliaji na ufugaji samaki katika kijijji cha Ilalasimba kata ya Nzihi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa amewaondoa hofu wakazi wa kijijji hicho kutokana na kuchelewa kwa ujenzi wa mradi huo wa kiuchumi uliofanyiwa upembuzi yakinifu tangu mwaka 2018.
Aidha Mhapa amesema ujenzi wa bwawa hilo litaongeza mapato ya kijiji hicho na wananchi kwa ujumla kutokana na shughuli zinazotarajiwa kufanyika.
Awali wananchi wa kijiji cha Ilalasimba wamesema walizuiwa kufanya shughuli zao ikiwemo kilimo katika eneo hilo kwa kipindi kirefu hali inayorudisha nyuma shughuli za kimaendeleo kwa kuwa hakuna ujenzi unaoendelea na kwamba wanaamini suala hilo linakwamishwa na siasa.