18 Mbaroni Kwa Wizi wa Mafuta
9 February 2023, 4:57 pm
Hii ni baada ya oparesheni iliyofanywa na jeshi la polisi mkoani Iringa kuanzia Jan 29 hadi Feb 5 mwaka huu
Na Hawa Mohammed.
Mafuta hayo, mipira 21 ya kunyonyea mafuta kwenye Malori, mapipa nane na chujio sita . Jeshi la Polisi mkoani Iringa Linawashikilia watu 18 akiwemo dereva wa Lori la mafuta (tank) Kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya mafuta ya Dizel na Petrol wanayodaiwa kuyapata kwa njia ya wizi.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP. Allan Bukumbi amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia oparesheni maalum iliyofanyika na kukutwa na madumu 158 ya mafuta aina ya Dizel Lita 482 na madumu matupu 305, piki piki mbili ambazo zilikuwa zikitumika kusafirisha
Aidha Kamanda Bukumbi amefafanua kuwa mbinu zinazotumiwa na wahalifu hao ni kuiba mafuta kwenye magari mbalimbali yanayoegeshwa pembezoni mwa barabara kuu ya Iringa – Morogoro, na wamekuwa wakishirikiana na Baadhi ya madereva wa magari ya kubebea mafuta kutoka makampuni mbalimbali kufanikisha wizi huo Kwa kunyonya mafuta na kuhamishia kwenye madumu yenye ujazo wa Lita 20 na kuendelea.
Hata hivyo Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa amesema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili na kutoa onyo Kali kwa wote wanaojihusisha na biashara hiyo huku akiwataka wananchi kuendelea kufichua wahalifu na uhalifu Katika maeneo yao .