Serikali kuimarisha sheria ya kodi
6 February 2023, 10:33 am
Tunaomba kuboreshwe kwa baadhi ya sheria za kodi hapa Nchini ambazo zinawabana wafanyabiashara.
Na Joyce Buganda
Serikali imeombwa kuendelea kuzingatia upya sheria za kodi ili kuimarisha uzalendo na ulipaji kodi wa hiari.
Hayo yamezungumzwa na naibu katibu Mkuu wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania BW. JAKSON KALOLO amesema baadhi ya taaratibu na Sheria za ulipaji kodi sio rafiki na zinakwamissha jitihada za kuipa kodi kwa wakati.
PAUL WALALAZE ni Meneja wa TRA mkoa wa iringa amesema mamlaka hiyo inashirikiana vyema na wafanyabiashara na kuwaomba kuendeleza ushirikiano huo ili kukuza uchumi wa nchi.
Walalaze amesema kuwa TRA iko tayari kutatua changamoto za Kibiashara kwa wafanyabiashara Mkoani Iringa.
“Sisi TRA Tunafanya kazi kutokana na malengo ambayo tumejiwekea na kwa kweli tunawapongeza wafanyabiashara ambao wamekuwa mstari wa mbele kulipa Kodi” alisema Walalaze
“Sisi TRA Tunafanya kazi kutokana na malengo ambayo tumejiwekea na kwa kweli tunawapongeza wafanyabiashara ambao wamekuwa mstari wa mbele kulipa Kodi” alisema Walalaze
Hivi karibuni akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani hapa waziri wa uwekezaji viwanda na biashara EXZAUD KIGAHE alisema kuwa serikali imeendeleza kuboreha sera na miongozo mbalimbali ili kurahisisha ulipaji wa kodi na kuimarisha sekta binafsi nchini.