Wazazi na walezi Iringa wahimizwa kutoa michango ya chakula shuleni
4 February 2023, 1:07 pm
Chakula kikiwepo shuleni kinasaidia kuondoa mazingira magumu kwa watoto na kupelekea wawe na utulivu wakati wa masomo na kukuza taaluma.
Na Ashura Godwin
Wazazi na Walezi mkoani iringa wametakiwa kuendelea kuchangia fedha kwa ajili ya chakula shuleni ili kuondoa mazingira magumu kwa watoto wawapo mashuleni na ili wawe na utulivu wakati wa masomo na afya bora.
Wakizungumza na nuru fm baadhi wa wazazi na walezi wamesema wazazi wanapaswa kutambua umuhimu wa wanafunzi kupata chakula shuleni kutokana na na kukaa muda mrefu bila ya kula hali inayosababisha kuwa na kiwango duni cha uelewa.
Kwa upande wake Afisa Taaluma Elimu Mkoa wa Iringa Mwl. Gervas Simbeye amesema ni jukumu la kila mzazi kuendelea kuchangia fedha za chakula ili kumfanya mwanafunzi kuwa na afya bora na utimamu wa akili.
Simbeye ameongeza kuwa zoezi la kutolewa kwa chakula mashuleni litasaidia kupunguza tatizo la utapiamlo na hivyo sheria zitaanza kuchukuliwa kwa wazazi ambao wataendelea kukiuka kwa agizo hilo.