Serikali yaombwa kuwasaidia watoto wenye ulemavu Iringa
2 February 2023, 3:07 pm
Serikali itupatie usaidizi wa namna ya kuwahudumia watoto wenye ulemavu Pindi wawapo shuleni kimasomo.
Na Fabiola Bosco
Wazazi wenye watoto walio na ulemavu Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wameiomba serikali kuwapa usaidizi wa namna ya kuwahudumia watoto wao pindi wawapo shuleni.
Wakizungumza na Nuru Fm baadhi yawazazi hao wamesema wamekuwa wakipitia changamoto mbalimbali pindi wanapowapeleka watoto shuleni kutokana upungufu wa walimu wenye uzoefu wa kuwahudumia watoto wenye ulemavu.
Kwa upande wake Afisa elimu wa Kata ya Isakalilo John Haruna amesema kuwa kila mtoto anahaki ya kupata elimu bila kujali upungufu alionao hivyo ni vyema wazazi kushirikiana na Viongozi wa serikali za mitaa ili fursa zinapotojitokeza wapewe kipaumbele.
“Utoaji wa taarifa unaweza pelekea wataalamu wakafika na kutambua ulemavu wa mtoto na kufahamu aina ya ulemavu alionao na shule anayopaswa kupelekwa kwa urahisi tofauti na kuwafungia ndani” alisema John.
“Utoaji wa taarifa unaweza pelekea wataalamu wakafika na kutambua ulemavu wa mtoto na kufahamu aina ya ulemavu alionao na shule anayopaswa kupelekwa kwa urahisi tofauti na kuwafungia ndani” alisema John.
Kila mtoto ana haki ya kupata elimu na huduma za msingi kama binadamu wengine huku Ripoti iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu na Sayansi (UNESCO) ya mwaka 2000-2015 inaonesha watoto wenye ulemavu milioni 58 hawapo shuleni duniani na watoto milioni 100 hawamalizi shule.
MWISHO