Askari 12 watunukiwa vyeti Iringa
31 January 2023, 12:02 pm
Askari waliotunukiwa vyeti vya utendaji kazi bora wamehimizwa kuwa wazalendo za kuzingatia haki pindi wanapotekeleza majukumu yao.
Na Elizabeth Shirima
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP. Allan L. Bukumbi amewatunuku vyeti vya pongezi Askari Polisi 12 na mtumishi raia mmoja kwa utendaji kazi bora katika majukumu ya kila siku kwa mwaka 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya FFU Kihesa Mjini Iringa, ACP. Bukumbi amesema kazi kubwa ya Askari Polisi ni kuzuia vitendo vya kihalifu katika kulinda raia na mali zao, kwa mwaka 2022 Iringa haikuwa na vitendo vya kutisha vya kihalifu kutokana na Askari na Maofisa walifanya kazi kubwa na ya ziada ya kuzima mitazamo ya kihalifu katika kuzuia vitendo hivyo.
Amesema kuwa askari wote wamefanya vizuri ila waliopewa zawadi ni wawakilishi kutoka kila eneo la utendaji kazi ambao wamefanya kazi vizuri zaidi.
“Hawa Askari waliopewa zawadi ni wawakilishi ambao wamefanya kazi vizuri zaidi kwa kujituma na kushirikiana na askari wenzao na wananchi katika kuhakikisha Iringa imekuwa salama kwa mwaka 2022” alisema Kamanda Bukumbi.
“Hawa Askari waliopewa zawadi ni wawakilishi ambao wamefanya kazi vizuri zaidi kwa kujituma na kushirikiana na askari wenzao na wananchi katika kuhakikisha Iringa imekuwa salama kwa mwaka 2022” alisema Kamanda Bukumbi.
Kwa Upande Wake Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na kuzuia Rushwa TAKUKURU mkoa wa Iringa Domina Mukama amewaasa polisi kutimiza viapo vyao na kutokujiingiza katika mikono ya Takukuru.