Watalii kufurahia utalii wa kulisha wanyama- Bateleur Safari yawaahidi furaha
16 December 2022, 5:38 pm
Utalii wa kulisha wanyama umetajwa kuwafurashisha zaidi watalii pindi wanapoenda katika ziara Hiyo ambayo safari hii itafanyika huko Jijini Arusha.
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Kitengo Cha Masoko kutoka kampuni ya usafirishaji watalii ya Bateleur Safari & Tours iliyopo Mkoani Iringa Bi. Jasmine Daniel na kuongeza kuwa utalii huo huwakutanisha watalii na wanyama ambao wamepewa mafunzo maalumu.
“Wanyama Hao kama Twiga, swala, Pundamilia na wengine wengi wamepewa mafunzo, pia Kuna uwezekano wa kupiga Picha na wanyama kama Simba na chui ambao ni ngumu watu kuwa nao karibu, niwasihi wanaotaka kufanya utalii huo wawasiliane nasi” Alisema Jasmine.
Amesema katika kutimiza azma Hiyo kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka, Kampuni yao imeandaa Safari ya kwenda Arusha iliyopewa jina la Tukalishe Twiga ambapo itahusisha watalii kutoka Iringa na Dodoma kuanzia tarehe 31/12/2022.
Amesema kuwa aliwahi kushiriki katika ziara ya kulisha wanyama, ambapo watalii waliokuwa katika Ziara Hiyo walifurahia huku wakisisitiza kuja na familia zako katika
ziara ya mwishoni mwa mwaka huu.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni Hiyo Rajipa David amesema kuwa wale watakaotaka kushiriki katika ziara Hiyo ya utalii ya kulisha wanyama watatakiwa kuchangia shillingi Laki Tano na elfu hamisini Kwa mtu mmoja na watalii wote watafurahia huduma zitakazotolewa.
“Gharama Hiyo itahusisha usafiri Kwa wanaoanzia Iringa na Dodoma, chakula, malazi katika hotel zote Ndani la Jiji la Arusha, gharama za kiingilio kwenda kwenye site zote, nyama choma na gharama za picha” alisema Rajipa.
Amesema Kwa wale wanaohitaji kushiriki katika ziara Hiyo ya utalii wanaweza kumpigia Kupitia namba za simu za 0765735261 Ili kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka Kwa kishindo.