Jeshi la Polisi Iringa lakamata Mtambo wenye thamani ya Mil 250 Mali ya Wizi
13 October 2022, 4:31 pm
JESHI la Polisi mkoa wa iringa limefanya operesheni na kukamata mtambo (wheel loader cartepille ) katika kijiji cha Igingilanyi kata ya isimani Wenye thamani ya Shilingi Million mia mbili hamsini .
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa ACP Allan Bukumbi amesema kuwa mtambo huo wenye namba T 322 CAF ni mali ya kampuni ya DB SHAPRIYA & COLTD.
Aidha ameongeza kuwa mtuhumiwa mmoja wa tukio hilo amekamatwa ambaye ni mwanaume mwenye umri wa miaka( 42) fundi na mkazi wa Nduli akiwa na mali za wizi zilizofunguliwa kutoka kwenye mtambo huo.
Hata hivyo mali alizokutwa nazo ni Engine model no 3126,Rejeta 01,Madguard 04,Hydrolic pipe,Wiring system pamoja na Fan Guard na Propeller shaft.
Katika tukio jingine ,jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata Pius Miki Mkazi wa wiloles kwa tuhuma ya kunja na kuiba katika nyumba ya ndugu yake Felix Miki ambapo baada ya mahojiano mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo na kuonyeshamali alizoiba katika nyumba hiyo.
Aidha vitu hvyo ni pamoja na Runinga aina ya Telefunken inchi 55,Jiko la umeme,Jokofu,Godoro,Sofa pamoja na mitungi ya gesi ya kampuni tofauti ambapo watuhumiwa watafikiwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.
MWISHO