Makalla awataka Vijana JKT kupambana na uhalifu
19 September 2022, 4:23 pm
Mkuu wa Mkoa wa Da es Salaam, Amos Makalla amefunga Mafunzo ya Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT, yaliyojulikana kama operesheni Jenerali Venance Mabeyo , huku akiwasihi vijana hao kuwa raia wema na kutojihusisha na vitendo vya uhalifu.
RC Makala, amefunga mafunzo hayo katika chuo cha Uongozi cha JKT kilichopo Kimbiji Wilayani Kigamboni, na kusema mafunzo hayo yamewajenga katika ukakamavu, uzalendo na weledi hivyo hatarajii kuona vijana hao 685 kujihusuha na vitendo visivyofaa katika jamii.
Amesema, “Tukapambane na vitendo vya uhalifu kwa nyie nilivyo waona panya road hawataweza hatucheki na panya road kwahiyo mkoa wowote utaokao enda wanamajina tofauti tofauti, Mbeya wanajina lao, Dodoma walioibuka jana wanajina lao hapa Dar es Salaam Panya road”
Aidha, RC Makalla amesema kuwa “niwahakikishie na wananchi mliopo gapa hatutocheka na kijana yeyote kwa umri wake eti ni mdogo tutashghulika naye”
Naye Mkuu wa Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji, Kanali Stanlaus Mishako amesema vijana hao wamemaliza mafunzo hayo ambapo wengi wao wanaendela na masomo katika vyuo mbalimbali wanatarajiwa kuwa mfano wa kuigwa katika jamii.
“Vijana wanajiamini wanajua kuwa hasa Kijana wa kitanzania anayejihusisha na ulevi, madawa ya kulevya, kuvunja sheria za nchi, kuwa na kiburi jeuri, tama kuwa na uchochezi na mambo mengine yote yasiokuwa na hali ya kuendana na mila zetu za kitanzania huyo ni mtu asiyestahili kupewa madaraka yoyote.
Aidha, amewasihi vijana hao yote waliyojifunza wakayaendeleze na wakawe mabalozi wazuri wa kulitangaza Jeshi la kujenga Taifa.