Rais Samia kuongoza Ujumbe wa Tanzania DRC
15 August 2022, 6:48 am
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atarajia kuwasili jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jumanne ya Agosti 16,2022, katika Mkutano wa kawaida wa 42 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Rais Samia anatarajia kuwepo nchini DRC, Kuongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano, ambapo tayari Mtanzania, Brigedia Jenerali Juma Nkangaa Sipe ameidhinishwa na Baraza la mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, kuwa Mkurugenzi wa asasi ya siasa, ulinzi na usalama katika sekretarieti ya SADC.
Brigedia Jenerali, Juma Nkangaa Sipe anachukua nafasi ya Ukurugenzi wa asasi ya siasa, ulinzi na usalama katika sekretarieti ya SADC, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi asasi hiyo Jorge Kodoso kutoka Jamhuri ya Angola, kumaliza kipindi chake cha miaka nane.
Tanzania imewasilisha pendekezo la la kufanyiwa marekebisho kwa Mkabata wa uanzishwaji wa SADC, ili kukitambua Kiswahili kisheria kama mojawapo ya lugha nne rasmi katika shughuli za SADC.