IRUWASA Kanda ya Kilolo yapeleka Maji Nyumba ya watu wenye ulemavu Kijiji cha Lulanzi
19 June 2022, 5:01 pm
Hatimaye mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Kanda ya Wilaya ya Kilolo imepeleka huduma ya maji safi ya bomba katika familia ya watu watatu wenye ulemavu iliyopo kijiji cha Lulanzi Kata ya Mtitu Mkoani Iringa.
Akizungumza mara baada ya huduma ya maji kufika katika nyumba hiyo, Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kilolo Wilson Nyangile amesema kuwa zoezi la kuwapeleka huduma ya maji limeshakamilika kwa zaidi ya wiki moja sasa.
Amesema kuwa kwa sasa ujenzi wa nyumba katika Familia hiyo unategemea maji ambayo tayari yamepelekwa kwa ushirikiano wa Balozi Isabella mwampamba, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Iruwasa Kanda ya Wilaya ya Kilolo pamoja na wadau wengine wa maendeleo.
Aidha Nyangile wamewataka wananchi kuendelea kutoa michango ili kukamilisha mradi wa ujenzi wa nyumba ambao kwa sasa uko katika hatua za mwisho kwa kuwasiliana na Mratibu wa zoezi hilo Isabella mwampamba kupitia namba 0762 756046 ili waweze kupewa utaratibu wa kutoa michango yao.
Naye Diwani wa Kata ya Mtitu Mh. Rahman Mkakatu amewapongeza Iruwasa kwa kufikisha huduma ya maji katika familia hiyo na kuongeza kuwa kwa sasa wanafanya utaratibu wa kuyaingiza maji hayo ndani ya nyumba ambayo inaendelea kujengwa kwa sasa.
Kwa upande wake mama mzazi wa walemavu hao Anjelista Kihanza amemshukuru balozi wa utalii Nchini Isabella mwampamba pamoja na serikali kwa ujumla kwa kuwasaidia kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili hasa ya maji kwani alikuwa akitembea umbali kufuata huduma hiyo.
Michango yote inapolokelewa kupitia acaount namba ya CRDB iliyosajiliwa kwa jina la Isabella African Foundation ya 015C621885600 huku Miradi hiyo ikitarajiwa kukamilika kwa muda wa miezi mitatu kwani imeanza kutekelezwa mwezi Mei mpaka Julai 2022 kwa kujenga nyumba, kuvuta huduma ya maji na kuwapatia malazi chakula na matibabu.