Nuru FM

Ofisi Ya Katibu Tawala Wilaya Ya Kilolo Yabariki Walemavu Lulanzi Kujengewa Nyumba Ya Kisasa

18 May 2022, 4:23 pm

Ofisi ya Katibu Tawala Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa imepokea wazo la Balozi wa Utalii Nchini Isabella Mwampamba kuwajengea nyumba ya kisasa walemavu watatu wa kijiji cha Lulanzi ili waweze kuwa na makazi bora.

 

Akizungumza katika ofisi yake Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Kilolo Wilson Nyangile amesema kuwa wanaunga mkono hatua ya kuwajengea nyumba hiyo ya kisasa baada ya Balozi Isabella kuwatembelea walemavu hao na kuona kuna uhitaji wa nyumba ya kisasa yenye vyoo ndani badala ya jiko.

Amesema kuwa watakaa kikao na watumishi wenzake ili kujadiliana kuhusu hatma hiyo huku akimshukuru Waziri Mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kuchangia shilingi Milioni tano kukamilisha mradi huo ambao kwa sasa umefikia hatua ya Msingi.

 

Aidha amesema kuwa fedha hizo zimeshawekwa katika akaunti ya wadau wa maendeleo ya Wilaya ya Kilolo na itatumika kununua vifaa vya ujenzi na kuwalipa mafundi ambapo amewataka wadau wengine kujitokeza kuwasadia walemavu hao ili waweze kuwa na malazi bora.

Kwa upande wao Diwani wa Kata ya Mtitu Mh. Rahman Mkakatu na Mwenyekiti wa Kijiji cha Lulanzi Bw.  Lucas Kihongosi wamesema kuwa mradi wa ujenzi huo unaendelea kwa kushirikiana na Shirika la RDO Wilaya ya kilolo ambao wametoa viijana kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa nyumba hiyo.

Hata hivyo wamewaomba wadau wa maendeleo kushiriki kuwasadia walemavu hao kwa kupeleka vifaa vya ujenzi, nguvu kazi na fedha kwa kuwasiliana na Mratibu wa zoezi hilo Isabella mwampamba kupitia namba 0762 756046 ili waweze kupewa utaratibu wa kushiriki kukamilisha miradi hiyo.

 

Walemavu hao wana uhitaji wa kuvutiwa maji, kujengewa nyumba ya kisasa, kupatiwa vifaa vya malazi, vifaa vya jikoni na gharama za chakula matibabu ambapo gharama zote ni shilingi milioni 20 na FEDHA zote zinapolokelewa kupitia acaount namba ya CRDB iliyosajiliwa kwa jina la Isabella African Foundation ya 015C621885600 huku Miradi hiyo ikitarajiwa kukamilika kwa muda wa miezi mitatu kuanzia mwezi Mei mpaka Julai 2022.