Nuru FM
Kupatwa kwa mwezi mei 15 na 16
15 May 2022, 1:02 pm
Siku ya leo mei 15 na Mei 16 huenda likatokea tukio la kupatwa kwa mwezi kwa mujibu wa utafiti wa NASA, ambapo mwezi utakua karibu na Dunia na utaonekana kwa ukubwa zaidi ukiwa na rangi nyekundu.
Kwa mujibu wa utafiti wa NASA imeandika tukio hilo litaonekana vizuri katika baadhi ya sehemu Duniani ambapo bara la Ulaya litaoneka kwa nchi za magharibi, bara la Marekani kaskazini, na Afrika.
Nusu ya Mashariki ya Marekani na Amerika Kusini watapata fursa ya kuona kila hatua ya kupatwa kwa mwezi.