Wakulima watumie viwanda
31 December 2020, 10:18 am
Naibu waziri wa viwanda na biashara mhe. Exsaud Kigahe, amewataka wawekezaji nchini, kuona umuhimu wa kujenga viwanda vya kuchakata mazao katika maeneo zinakopatikana kwa wingi malighafi zitokanazo na kilimo.
Mhe. Kigahe amesema hayo wakati alipowatembelea wakazi wa kata ya mapanda wilaya ya mufindi mkoani iringa nakueleza kuwa endapo viwanda vya kuchakata mazao vitajengwa katika maeneo hayo, mazao yataongezewa thamani na hivyo kumuepusha mkulima na hasara ya mazao yake huharibikia njiani – jambo ambalo hupupunguza thamani ya mazao hayo kuingia viwandani
Nao wakazi wa Kata ya Mapanda Mufindi mkoani Iringa, wamemueleza naibu waziri huyo kuwa mazao yao hukosa wanunuzi, kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara, jambo linalochangia wafanyabiashara wasifike kununua mazao na kutokifikia kuwa na kilimo chenye tija.
.