Nuru FM

Lissu atakiwa kuzisemea changamoto Cha wananchi

23 January 2025, 11:26 am

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Tundu Lissu akizungumza baada ya kutangazwa mshindi. Picha na Ayoub Sanga

Na Cleef Mlelwa

Wanachama wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mjini Makambako wamemtaka Mwenyekiti wao Tundu Lissu kuhakikisha wanajenga ofisi zake na kuwa tumaini kwa wananchi kwa kuzisemea changamoto zinazoikabili jamii hasa katika sekta ya afya,elimu na kilimo.

Wakizungumza na Kituo hiki baadhi ya wanachama wa chama hicho mjini Makambako wamesema mara baada ya Lissu Kutangazwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho matarajio yao ni kuona anarejesha umoja na mshikamano ndani ya chama na kuhakikisha kinakuwa na ofisi zake kila kata na jimbo.

Sauti ya Wanachama

Aidha katibu wa chama cha Act Wazalendo Stanely Mbembati amesema ushindi wa Tundu Lissu utasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha vyama vya upinzani kwa kuwa amekuwa na misimamo ambayo itasaidia kuchukua hatua zaidi badala ya kuishia kufanya maridhiano yasiyo na tija.

Sauti ya Act wazalendo

Mwenyekiti wa chadema wilaya ya Njombe Seth Vegulla amesema licha ya mwenyekiti huyo taifa Tundu Lissu kuja na mikakati ya kuhakikisha uchaguzi una kuwa huru pia anakazi ya kuhakikisha chama hicho kinakuwa na katiba imara ambayo itakuwa na ukomo wa madaraka kwa viongozi wa chama hicho.

Sauti ya Mwenyekiti

Naye katibu wa chadema Mkoa wa Njombe amesema uchaguzi wa chama hicho umeonyesha nini maana ya demokrasia kwa vyama vyote vya kisiasa nchini na kueleza kuwa kupitia misimamo ya mwenyekiti wao hakutakuwa na maridhiano tena zaidi ya kufanya maamuzi.

Sauti ya Katibu

Tundu Lissu ametangazwa kuwa mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema taifa baada ya kupata kura 513 sawa sawa na asilimia 51.5,huku mpinzani wake Freeman Mbowe akipata kura 482 sawa na asimilia 48.3 na Charles Odero akipata kura moja sawa na asilimia 0.1.

MWISHO