Wadau wa mazingira na utalii kuja na mpango wa kutunza vivutio vya asili
23 January 2025, 11:50 am
Na Joyce Buganda
Wadau wa Mazingira na utalii wametakiwa kuwa mabalozi kwa kutunza vivutio vya asili ili jamii inayowazunguka iige mfano kutoka kwao
Akizungumza wakati akifungua warsha ya siku mbili iliofanyika katika ukumbi wa hotel ya Sunset Iringa mjini Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Joachim Nyingo ambae alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Iringa amesema kampeni hii inalenga kutunza na kuuhifadhi mlima udzungwa kwa kuwa ni jukumu la Kila mtu.
Meneja mradi wa mradi wa mpango mkakati wa kuhifadhi ya mlima Udzungwa UDZUNGWA LANDSCAPE STRATEGY Arafat Mtui amesema lengo kuu ni kuboresha shughuli za uhifadhi katika hifadhi tatu ikiwemo hifadhi ya milima ya udzungwa pamoja na kuboresha uhusiano mzuri kati ya wananchi waliozunguka hifadhi hiyo.
Kwa upande wake Afisa wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na utalii Bi. Rose Mdendemi amesema mkakati wa serikali ni kupunguza migongano baina ya wanyamapori na binadamu lengo kuu ni kutunza Mazingira.
Warsha hii imeandaliwa na wadau pamoja na mashirika mbalimbali kama STEP, MAZINGIRA na REFOREST AFRICA lengo kuu likiwa ni kutunza Mazingira hasa yanayozunguka hifadhi za Taifa ikiwemo hifadhi ya mlima ya udzungwa.
MWISHO